Francis Mtalaki
Francis Mtalaki alijiunga na KTN Machi 2013 na kupata mafunzo ya kazi kwa muda wa miezi sita kabla ya kupokea kandarasi ya kufanya kazi na KTN. Amezuru kaunti mbali mbali humu nchini kama vile kaunti za Kajiado, Taita Taveta , Murang’a, Garissa na nyinginezo.
Katika muda huu ameweza kuangazia taarifa tofauti kutoka nyanja mbalimbali kama vile maswala ya afya, siasa, yanaojiri, wanachopitia familia vitongojini na hata tamaduni za jamii tofauti humu nchini.