Francis Mtalaki

Image of Francis Mtalaki

Francis Mtalaki alijiunga na KTN Machi 2013 na kupata mafunzo ya kazi kwa muda wa miezi sita kabla ya kupokea kandarasi ya kufanya kazi na KTN. Amezuru kaunti mbali mbali humu nchini kama vile kaunti za Kajiado, Taita Taveta , Murang’a, Garissa na nyinginezo.

Katika muda huu ameweza kuangazia taarifa tofauti kutoka nyanja mbalimbali kama vile maswala ya afya, siasa, yanaojiri, wanachopitia familia vitongojini na hata tamaduni za jamii tofauti humu nchini.

Alizaliwa na kusomea katika kaunti ya Taita Taveta kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Nairobi jijini Nairobi kusomea Taaluma ya Uanahabari kati ya mwaka 2008 hadi 2012 alikotoka na Shahada ya Uanahabari.