Lofty Matambo

Image of Lofty Matambo

Lofty Matambo alijiunga na KTN mwishoni mwa mwaka wa 2013.

Awali mwaka wa 2013 alikuwa mtayarishi msaidizi na mwelekezi wa makala ya kipindi cha Tazama chini ya shirika la Media Development in Africa (MEDEVA) yaliyokuwa yakipeperushwa kwa runinga ya KTN. Alipata fursa ya kuzuru kaunti mbali mbali nchini kama vile Garissa, Kilifi, Kwale, Lamu, Marsabit na nyenginezo.

Alikuwa pia mtangazaji wa kujitolea wa kipindi cha Tumaini Maishani cha nyimbo za injili katika kituo cha Pwani FM, Mombasa mwaka wa 2012

Akiwa KTN matambo ameangazia habari na makala yanayogusia maisha ya binadamu, yakiwemo magonjwa, familia za mitaani, ugumu wa malezi, wazazi katili na kadhalika. Amezuru maeneo yanayozongwa na vita vya kimbari na ugaidi kama vile Marsabit, Samburu, Isiolo na Mandera. Matambo pia hukuletea makala ya Wako Wapi ambayo huangazia walikopotelea watu mashuhuri na wasanii, kila Jumapili saa moja jioni.

Tuzo: KEMEP Awards - Best Reporter 2013: Gender and Development

Uraibu: Kuzuru maeneo mapya, kuimba na kudensi