Saida Swaleh

Image of Saida Swaleh
Saida
Swaleh
Twitter ID
SaidaSwaleh
Facebook Fan Page
https://www.facebook.com/sriyami

Saida Swaleh alijiunga na KTN Aprili 2011. Saida ni mahafala wa shahada ya Mawasiliano na Uandishi Habari, chuo kikuu cha Nairobi . Uanahabari ni kazi aliyoisomea kwa hima na sasa amefanikiwa kuwa mwanabari anayebobea haswa katika uandaaji makala.

Saida amepata tuzo nyingi tangu kujiunga na KTN. Anatambulika katika kuangazia maswala ya afya, hasa ya akina mama na watoto.

Amejenga tajriba aliyonayo sasa kwa kusafiri katika nchi nyingi kuandaa taarifa kuhusu maswala tofauti tofauti. Hali hii imemwezesha kuingia kwenye ulingo wa makala marefu (long form/documentary reporting).

Saida anaipenda kazi yake na ana kila nia kujiboresha kupitia masomo ya zaidi ili kuiendeleza.

Anatia tamati kwa kusema kwamba yeye ni mke na mama ya mtoto mmoja, anawapenda wote kwa dhati … anaamini kuwa pasipo wao maishani mwake, asingekuwa Saida Swaleh hii leo.